Wednesday, 24 February 2016

KUSIMAMA KWENYE ZAMU YANGU

MCH.KIONGOZI: L.A.WILLIAM
SOMO: KUSIMAMA KWENYE ZAMU YANGU.

Kila mwanadamu ana zamu zake katika maisha ya kawaida ambazo Mungu ameziweka katika maisha.
ilitupasa wanadamu kisimama katika zamu zetu(nafasi) ili kutimiza kusudi husika la Mungu katika maisha yetu.

                Habakuki 2:1
   mimi nitasimama katika zamu yangu,nitajiweka juu ya mnara,nitaangalia ili nione atakaloniambia,na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.

      wanadamu wengi upenda kulalamika na kunung'unika mbele za Mungu badala ya kusimama katika zamu zao.
       jua siri hii yapo mashetani yanayopenda watu wa Mungu walie machozi ya kulalamika na kwao yawe kama kinywaji.
        wakristo wengi awapendi kusimama katika nafasi zao bali wanapenda kuuliza kwa waombaji juu ya shida zao....kanakwamba mganga wa kienyeji na mteja wake.

         unaposimama katika zamu yako juu ya tatizo lako nirahisi tatizo kuisha sababu umesimama katika zamu yako kuomba.

♡KILA MWANADAMU ANAZAMU YAKE KATIKA MAISHA.

           Mashetani wanajua mtu aliesimama katika zamu yake(nafasi) na kuitumia vizuri na shetani anamuogopa sana mtu anaejitambua.

       wachawi wanazamu zao usiku kuloga nawe ikifika usiku weka zamu yako ya kuomba.

     Tatizo linapokuwa kubwa sana kwako ndo wakati wakusimama katika zamu yako kushinda nalo.

       tamali alisimama katika zamu yake kama mke akamuokoa daudi mumewe...
simama katika zamu yako utapata jibu la shida yako.

                    luka 19:41-44
       Alipofika karibu aliuona mji,akasema,Laiti ungalijua,hata wewe,katika siku hii,yapasayo amani!.......
        anasema laiti ubgelijua majira na wakati ungesimama katika zamu yako na adui asingekujengea bomaa.
        Roho Mtakatifu anahemu zamu yako inakupasa kusimama kama nikuonya onya kama nikuomba omba n.k

     kila mwenye karama Mungu usema nae na kumtumia pale anaposimama katika zamu zao.

                         yona 1:6
      Basi nahodha akamwendea,akamwambia,una nini,Ewe ulalae usingizi?amka,ukamuombe Mungu wako,...........

MUHIMU KUSIMAMA KATIKA ZAMU YAKO.

MAWASILIANO :0784 986631,0653 830567
     
      

No comments:

Post a Comment