SNP.L.A WILLIAM 21/02/2016 ZAKARIA 4:6-7 ipo siri katika milima,kuna milima ya mwilini na milima ya rohoni. 2 WAFALME 23:13-26 jua siri hii unapoona jambo limekaa upande la kulia kwako maanake linasababu kwanini likae hapo na lina haki ya kukaa hapo na lina nguvu ya kutumia haja yake. Ndio maana katika koo zetu kuna sehemu ambayo miungu ya ukoo inakaa milimani wanawezo wa kuhukumu wakiwa mlimani,kukufunga,kukulaani,wakiwa milimani na wananguvu sana wakiwa milimani na zipo madhabahu milimani. Kuna milima iliyowekwa kabisa ambayo shetani ameichagua kwa ajili ya kazi zake kwa mfano:- ZABURI 2:6 Mungu aliweka ufalme wake mlimani ili ufalme uwe na nguvu lazima kukaa mlimani.Mungu aliumba milima kama sehem maalumu ili watu waweze kusema nae milimani kumbuka musa alisema na Mungu milimani,Yesu nae alikuwa anaomba milimani ili kusema na Mungu. Musa alipanda mlimani akaongea na Mungu,akapewa amri kumi milimani alimuona Mungu mlimani. siri ya milima ni kuzungumza na Mungu kwa upesi. EZEKIELI 28:14 hata shetani alivoasi aliamua kueka madhabahu nyingi milimani. mfano..inchi ya Tanzania baada ya uhuru bendera ilipandishwa mlimani(kilimanjaro). Pia Mungu anapenda kutukuzwa kutoka milimani ndo sababu kumueka lussifa akae milima ya moto ili amtukuze kutokea apo. Kuna baadhi ya milima inamasharti yake mingine unapanda kimya kimya mfano milima ya matambiko ya ukoo na milima ya uganga na uchawi. Koo ambazo zinaabudu milimani ni ko ambazo zinanguvu sana na hukumu kali sana iyo ni siri ya milima. SHUHUDA YA MTU ALIEKUWA WANAABUDU MILIMANI KATIKA KOO YAO.(angalia picha na maelezo chini) Wakuu ya koo izo wanauwezo wa kupanda milimani ili kuhukumu ili kufunga maisha ya watu iyo yote Mungu anaiita MILIMA YA UHARIBIFU. Na shetani kafunga koo nyingi kwenye milima na uwa wanatoka sadaka milimani(mbuzi n.k). Milima ya uharibufu kazi yake ni kuharibu. MATHAYO 4:8 Shetani alimchulua Yesu adi milimani ili amuoneshe miliki za ulimwengu ila lengo la shetani amfanye Yesu amuinami ila kristo alimshinda. Maana alikuja kuimalisha ufalme usiotikisika. Unapo abudu katika milima ya uharibifu unakuwa upo chini ya milima iyo. OMBI:KUKATAA NA KUJIONDOA KATIKA MILIMA HIYO. YEREMIA 51:25 Kwahiyo dunia nzima imaharibiwa na milima hii ya uharibifu. mfano…Inchi ya china ni inchi wanao abudu milimani na inakuwa nguvu sana. Baada ya kujua siri za milima apo unaweza pambana na nguvu zilizopo uko. Morogoro ni mji wenye milima mingi na ndo mji wenye waganga wa kienyeji na uchawi mzito sababu ya milima. Nakuna watu wanakula wadudu na wanyama na vitu kutoka milimani. Hata kwenye maisha ya kawaida ya wanyama na wao wanajitenga milimani (simba na simba mlimani kwao. n.k). OMBI: KUTEKETEZA MILIMA YA UHARIBIFU. HAGAI 1:8 Mungu anaangalia milima ili utoe miti ya kumtukuza yeye kwa kufanya kazi yake( kujengea nyumba yake). Ipo milima ya rohoni mfano: ya umaskini,magonjwa,tabu,laana n.k. Yesu alizaliwa katika familia iliyomaskini ili sisi tushuke katika milima ya umaskini tukae katika utajiri. Mungu alitoa watumishi wake kutoka milimani kwenye tabu,dhambi,magonjwa ili awatengeneze wawe watumishi wake wakweli ndio o watumishi wengi wametoka katika milima tofauti tofauti na sasa wanamtukuza Mungu. Wakati mwingine Mungu anaruhusu upite katika milima ya uharibifu ujifunze ili ukija kwa tika njia yake umtukuze katika roho na kweli.Mungu anapenda vichafu ili avitusafishe zimtukuze. OMBI: BWANA NITENGENEZE NA MIMI NIWE CHOMBO CHAKO. yesu alipenda kuomba milimani. EZEKIEL 35:11-15.
MAWASILIANO: 0784 986631,0653 830567.
No comments:
Post a Comment