MCH.KIONGOZI: L.A.WILLIAM.
SOMO:TUMEHESABIWA HAKI ZOTE KWA NEEMA SI KWA MATENDO.
kuna wakati kwenye maisha tunapita kwenye kipindi tunavuka katika tabu na magumu wengi wanawaza sababu wao wanahaki ndo mana wanavuka kumbe ipo neema inayo leta haki.
hatuna sababu ya kujivuna maana atufanyi kwa akili wala kwa nguvu ila ipo neema inayoleta haki kwetu.Mungu amerihusu haki itufuate ni kwa Neema yake tu.
Neema utuokoa,neema utubeba,neema utuvusha,neema uleta haki. yote ni kwa neema.
kuna wakati tulitakiwa kufa ila neema imetuokoa.
NEEMA ULETA WOKOVU
NEEMA ULETA HAKI
NEEMA UTUFIKISHA HAPA TULIPO.
warume 3:21-24
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake,kwa njia ya ukombozi ulio katika kristo yesu.....
kumbe atupaswi kujivuna kujiinua sababu ya neema tuliyopewa...
kuna wakati Mungu uruhusu mtu apite katika magumu ili ajifunze kutulia katika mikono ya Mungu.vyote si vyetu yule mwenye navyo alietupa sisi.
ukiona kuna jambo lolote linakuwa gumu uweI kulifanya au alitimii basi muombe Mungu neema ya kulitimiza jambo ilo.
1 wakorintho 15:10
lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa ivi nilivyo;na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure,bali nilizidi sana kufanya kazi kupita wao wote;wala si mimi,bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
paulo anasema wazi juu ya neema ya Mungu kwake.Anasema hana haja ya kujisifu kwa kuwa alifanya kazi kupita wote ila anagundua mi neema ndio iliyo mfanya aweze kufanya yote.
Haraka ya mwanadamu aifanyi mapenzi ya Mungu.bali yeye mwenye subira kwa Bwana atakula ya Bwana.
wagalatia 2:21
siibatili neema ya Mungu;maana,ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria,basi kristo alikufa bure.
vyote ndoa,kuzaa,baraka, ni kwa neema wala si sheria. muhimu kutunza neema ya Mungu katika maisha.
waefeso 1:3-6
Atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni,katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo..........
tumechagulia kwa neema.
mawasiliano:0653 830567,0784 986631
fbpage: the harvest of jesus christ church int.
gmail: theharvestofjesuschrist@gmail.com
youtube: hcc international tv
No comments:
Post a Comment